Posts

Showing posts from May, 2019

Kocha wa Simba SC asaini mkataba mpya

Image
Kocha wa Simba SC, Patrick Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo. Uamuzi wa kumuongezea mkataba umeafikiwa na Bodi ya Wakurugenzi baada ya Kocha Aussems kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni ya kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu na inafika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

JKT wajipanga fainali ndogo ya mwisho dhidi ya Stand United

Image
Kocha wa JKT Tanzania, Mohamed Abdallah 'Bares' amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya fainali ndogo ya mwisho dhidi ya Stand United itakayochezwa Uwanja wa Isamuhyo, Mei 28. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuwa kwenye hatari ya kushuka Daraja msimu ujao. JKT imecheza michezo 37 ina pointi 44 ikiwa nafasi ya 13 huku mpinzani wake Stand United akiwa nafasi ya 14 na ana point 44 kama zake. Bares amesema anaheshimu timu zote zilizo kwenye ligi, hivyo ataingia uwanjani kwa mikakati ya kutafuta ushindi mapema ili kushusha presha ya kupoteza pointi tatu muhimu. "Ni mchezo mgumu na utakuwa ni zaidi ya fainali kutokana na nafasi ambayo tupo ila hakuna namna, nimejipanga kupata matokeo chanya mbele ya wapinzani wangu kikubwa ni pointi tatu muhimu, mashabiki watupe sapoti," amesema.

Iran yaapa kujilinda kwa nguvu zote dhidi ya uchokozi

Image
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif, amesema nchi yake inajilinda kwa nguvu zote dhidi ya uchokozi wa kijeshi na kiuchumi, huku akizitolea wito nchi za Ulaya kuchukua hatua zaidi kuyanusuru makubaliano ya nyuklia waliyotia saini. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini Baghdad, Iraq, hivi leo, Zarif amesema nchi yake inataka kujenga mahusiano ya usawa na jirani zake wa eneo la Ghuba na imekwishapendekeza kutiwa saini mkataba wa kuepuka uchokozi. Wakati huo huo, Rais Hassan Rouhani wa Iran ameashiria kuwa Iran inaweza kuitisha kura ya maoni kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo kufuatia kuongezeka mvutano kati yake na Marekani. Rouhani amesema amewahi kupendekeza suala hilo kwa Kiongozi wa Mkuu Ayotallah Ali Khamenei mwaka 2004 alipokua mjumbe mwandamizi kwenye mazungumzo ya nyuklia. Kura hiyo ya maoni itaipa serikali ya Iran uhalali wa kisiasa iwapo itaamua kuongeza urutubishaji wa madini ya urani unaozuiwa chini ya makubaliano ya 2015 na mataif...

Kocha wa Yanga SC ashikilia mikataba ya wachezaji 14

Image
Uongozi wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna presha na wachezaji ambao utawafanyia usajili msimu ujao kwani tayari kazi hiyo wamemuachia kocha mkuu, Mwinyi Zahera ambaye anashughulikia mafaili yote ya wachezaji. Yanga mpaka sasa wachezaji wake 16 wa kikosi cha kwanza wanamaliza mikataba yao msimu huu hivyo kinachosubiriwa ni kuwaongezea mkataba wale ambao watakidhi vigezo vya kocha. Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa hawashughuliki na masuala ya usajili kazi hiyo wamemuachia Zahera. "Kuhusu usajili sisi tupo vizuri kwanza tunaanza na wachezaji ambao mikataba yao inamalizika na wameonyesha kazi kubwa na kocha akawakubali hivyo hatma yao ipo mikononi mwa Zahera," amesema Mwakalebela. Wachezaji ambao inaelezwa kwamba mikataba yao inakwisha msimu huu ni pamoja na Ramadhani Kabwili,Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma Makapu, Matheo Anthony, Thabani Kamusoko, Raphael Daudi,...

RC Njombe aweka utaratibu wa haki kwa wote wanaotumia Stendi mpya ya mabasi

Image
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amefanya ukaguzi katika kituo kituo kipya cha mabasi kitakachogharimu zaidi ya bil 9.6 pamoja na ujenzi wa mradi wa soko kuu mjini Njombe lenye hadhi ya kimataifa litalogharimu bil 9.3 na kuonyesha kuridhishwa na mwenendo wa ukamilishaji wa miradi hiyo inayofadhiliwa na benk ya dunia. Lakini pamoja na kuridhishwa na ujenzi unaoendelea akiwa katika kituo cha mabasi ambacho kilianza kufanya kazi mai 10 kwa agizo la rais ,mkuu wa mkoa amepokea malalamiko kutoka kwa abiria,machinga,mama na baba lishe ambao wanasema wanashindwa kufanya biashara kama ilivyokuwa awali katika stendi ya zamani kwani halmashauri imezuia kufanya biashara ndani ya stendi hata kwa wenye vitamburisho vya mjasiriamali Mara baada ya kusikiliza kero hizo Christopher Olesendeka anatoa kauli ili kuweka utaratibu wa haki kwa wote wanaotafuta liziki yao katika kituo cha mabasi ambapo anamtaka mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Illuminata Mwenda kupeleka kwake mpa...

Madiwani Halmashauri za Mijini na Vijijini wanolewa kuhusu maadili ya Viongozi wa Ummma

Image
Na Timothy Itembe, Mara. Madiwani pamoja na Watumishi wake wa Halmashauri za Tarime Mjini na Vijijini mkoani Mara wamenufaika na semina ya siku Moja iliyoandaliwa na Sekreterieti ya maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya Ziwa ikiwataka kutekeleza majukumu, Mamlaka na misingi ya maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa sheria. Katibu msaidizi wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma kanda ya Ziwa Godson Peter Kweka alisema kuwa Sekretarieti ina jukumu la kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi yeyote wa umma ambaye ameorocheshwa katika sheria ya maadili ya viongozi wa umma pamoja na wale wameongezwa kwa mjibu wa sheria kwa madhumuni ya kuhakikisha masharti ya sheria hiyo yanazingatiwa. "Maadili yana umuhimu mkubwa katika utawala na maendeleo ya Nchi kutokuwepo kwa uwadilifu kunaongeza hatari (risk) ya Rushwa ubadhilifu matumizi mabaya ya mali za umma wizi kwa hali hiyo maadili  ni kinga mhimu ya maovu  yote"alisema Kweka. Kweka aliongeza kuwa kiongozi wa umma ha...