Madiwani Halmashauri za Mijini na Vijijini wanolewa kuhusu maadili ya Viongozi wa Ummma
Na Timothy Itembe, Mara.
Madiwani pamoja na Watumishi wake wa Halmashauri za Tarime Mjini na Vijijini mkoani Mara wamenufaika na semina ya siku Moja iliyoandaliwa na Sekreterieti ya maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya Ziwa ikiwataka kutekeleza majukumu, Mamlaka na misingi ya maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa sheria.
Katibu msaidizi wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma kanda ya Ziwa Godson Peter Kweka alisema kuwa Sekretarieti ina jukumu la kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi yeyote wa umma ambaye ameorocheshwa katika sheria ya maadili ya viongozi wa umma pamoja na wale wameongezwa kwa mjibu wa sheria kwa madhumuni ya kuhakikisha masharti ya sheria hiyo yanazingatiwa.
"Maadili yana umuhimu mkubwa katika utawala na maendeleo ya Nchi kutokuwepo kwa uwadilifu kunaongeza hatari (risk) ya Rushwa ubadhilifu matumizi mabaya ya mali za umma wizi kwa hali hiyo maadili ni kinga mhimu ya maovu yote"alisema Kweka.
Kweka aliongeza kuwa kiongozi wa umma hatakiwi kuingia mikataba ya kibiashara na taasisi iliyo chini ya usimamizi wake pia kiongozi huyo anatakiwa kutokuwa na mwenendo ambao utaaibisha utumishi wa umma baada ya kuacha wadhifa husika.
Katika semina hiyo diwani kata ya Bumera wa halmashauri ya Tarime vijijini kupitia Chama cha mapinduzi CCM,Deogratius Ndege alisema kuwa semina hiyo imewajenga na kuwa viongozi waliowengi walikuwa hapo nyuma wakifanya kazi huku wakiingilia majukumu ya viongozi wengine.
Ndege aliongeza kuwa Majukumu na Mamlaka na misingi ya maadili ya viongozi wa umma iliyopo kwa mjibu wa sheria ikitekelezwa vizuri itakuwa imesaidia kutekeleza sera ya Serikali ya wamu ya Tano ya Rais John Pombe Mafuguli ya Tanzania mpya na Tanzania ya viwanda.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime Mjini,Hamis Ndera ambaye ni diwani kata ya Sabasaba kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema alisema kuwa semina hiyo ni nzuri lakini imekuja nje ya wakati kwani baadhi ya viongozi wa umma kwa maana ya madiwani wanenda kumaliza mda wao wa uongozi waliopewa na wananchi waliowachagua kwa mjibu wa sheria kuwatumikia.
Naye mkuu wa wilaya Tarime mkoani hapa,Charles Kabeho alisema kuwa kiongozi wa umma anatakiwa kutamka masilahi binafsi aliyonayo juu ya suala linalojadiliwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri,Bunge au kamati zake na Baraza la madiwani au kamati zake na kuwa kiongozi wa umma anatakiwa kutojiingiza katikas vitendo vya Rushwa au matumizi yoyote mabaya ya madaraka au wadhifa.
Kabeho aliongeza kuwa kila kiongozi anatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa mjibu wa sheria zilizopo huku akitatua kero za wananchi bila kujali itikadi ya vyama vya siasa wala upendeleo wowote huku wakitanguliza masilahi mapana na Taifa.
Comments
Post a Comment