JKT wajipanga fainali ndogo ya mwisho dhidi ya Stand United
Kocha wa JKT Tanzania, Mohamed Abdallah 'Bares' amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya fainali ndogo ya mwisho dhidi ya Stand United itakayochezwa Uwanja wa Isamuhyo, Mei 28.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuwa kwenye hatari ya kushuka Daraja msimu ujao.
JKT imecheza michezo 37 ina pointi 44 ikiwa nafasi ya 13 huku mpinzani wake Stand United akiwa nafasi ya 14 na ana point 44 kama zake.
Bares amesema anaheshimu timu zote zilizo kwenye ligi, hivyo ataingia uwanjani kwa mikakati ya kutafuta ushindi mapema ili kushusha presha ya kupoteza pointi tatu muhimu.
"Ni mchezo mgumu na utakuwa ni zaidi ya fainali kutokana na nafasi ambayo tupo ila hakuna namna, nimejipanga kupata matokeo chanya mbele ya wapinzani wangu kikubwa ni pointi tatu muhimu, mashabiki watupe sapoti," amesema.
Comments
Post a Comment