RC Njombe aweka utaratibu wa haki kwa wote wanaotumia Stendi mpya ya mabasi
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amefanya ukaguzi katika kituo kituo kipya cha mabasi kitakachogharimu zaidi ya bil 9.6 pamoja na ujenzi wa mradi wa soko kuu mjini Njombe lenye hadhi ya kimataifa litalogharimu bil 9.3 na kuonyesha kuridhishwa na mwenendo wa ukamilishaji wa miradi hiyo inayofadhiliwa na benk ya dunia.
Lakini pamoja na kuridhishwa na ujenzi unaoendelea akiwa katika kituo cha mabasi ambacho kilianza kufanya kazi mai 10 kwa agizo la rais ,mkuu wa mkoa amepokea malalamiko kutoka kwa abiria,machinga,mama na baba lishe ambao wanasema wanashindwa kufanya biashara kama ilivyokuwa awali katika stendi ya zamani kwani halmashauri imezuia kufanya biashara ndani ya stendi hata kwa wenye vitamburisho vya mjasiriamali
Mara baada ya kusikiliza kero hizo Christopher Olesendeka anatoa kauli ili kuweka utaratibu wa haki kwa wote wanaotafuta liziki yao katika kituo cha mabasi ambapo anamtaka mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Illuminata Mwenda kupeleka kwake mpango kazi wa uendeshaji na utoaji wa dhabuni katika stendi hiyo ili kuepusha malalamiko kwa watumiaji
Katika hatua nyingine Olesendeka amekagua ujenzi wa soko kuu ambao anaonyesha kuridhishwa na kasi na ubora katika ujenzi huku eng wa mradi huo Mboka jastin akidai mradi umefika asilimia 60 na kuahidi kukamilika ndani ya muda uliopangwa.
Comments
Post a Comment