Kocha wa Simba SC asaini mkataba mpya
Kocha wa Simba SC, Patrick Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo.
Uamuzi wa kumuongezea mkataba umeafikiwa na Bodi ya Wakurugenzi baada ya Kocha Aussems kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni ya kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu na inafika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Comments
Post a Comment