jifunzebure 4 years ago Advertisements Katika hatua hii ya kwanza utajifunza kuhusu kampuni ya Microsoft na historia fupi ya waanzilishi wake. Utajifunza sehemu kuu za kompyuta ambazo ni KIU (Kitengo kikuu cha uchakataji) au CPU (Central Processing Unit), Monita, puku, bodidota na printa. Mfululizo wa masomo haya utakujengea msingi wa kuanza kutumia kompyuta hasa matumizi ya programu za Microsoft ofisi kama vile Microsoft Word, Microsoft powerpoint, Microsoft publisher, Microsoft Excel n.k. Mpaka mwisho wa somo hili utujua: Historia fupi ya Kampuni ya Microsoft na waanzilishi wake Sehemu kuu za kompyuta Kuhusu kampuni ya Microsoft Kampuni ya Microsoft ni kampuni ambayo hutengeneza programu za kompyuta kwa ajili ya watumiaji wa kompyuta duniani kote. Ilianzishwa mnamo mwaka 1975 na Bill Gates kwa kushirikiana na Paul Allen. Programu ambazo hutengenezwa na kampuni hii ni pamoja na windows, Microsoft office (kama vile, Microsoft word, Powerpoint, Pu...
Comments
Post a Comment