Jinsi ya kutatua tatizo la “Download pending” kwenye Playstore. #Maujanja
@huduma
Simu janja (rununu) tunazotumia hasa kwa wale tunaotumia simu za Android tunakumbana na matatizo mengi lakini ambalo tunakutananalo ni “Download pending” pale unapojaribu kupakua/kufanya masasisho ya programu tumishi.
Unaweza ukafikri kuwa umeishiwa na kifurushi cha intaneti na ndio maana ukijaribu kushusha kitu kutoka kwenye soko la programu tumishi za Android maarufu kama Playstoreinakataa huku bado ukiwa na salio la kutosha.
“Download pending” ni tatizo ambalo linatokana na kuwepo kwa nafasi finyu ya Playstore kuweza kukubali data za programu tumishi nyingine.
Jinsi ya kutatua tatizo la “Download Pending” kwenye simu za Android.
Tatizo hilo unaweza ukafikiri kuwa ni vigumu sana kuondoa lakini la hasha! Unatakiwa kufanya kitu kidogo tu; ingia settings>>apps>>Google Playstore>>App info kisha bofya “Clear Data“.
Comments
Post a Comment